Friday , 15th Jun , 2018

Baada ya Yanga kutuma barua ya kuomba kujitoa kwenye michuano ya Kombe la Kagame, hatimaye shirikisho la soka kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), limekubali ombi hilo na kuipa nafasi timu ya Vipers kutoka nchini Uganda.

CECAFA imeamua kuwaalika Vipers SC ya Uganda kuchukua nafasi ya Yanga ambapo wataungana na timu zingine za kundi C  Simba, Dakadaha ya Somalia na St. George ya Ethiopia.

Michuano hiyo ambayo inatarajiwa kuanza June 28 mwaka huu na kumalizika Julai 13 2018 , itashirikisha timu 12 kutoka Afrika Mashariki pamoja na timu waalikwa. Pia itachezwa kwenye viwanja viwili, uwanja wa Taifa na Chamazi Complex.

Timu hizo zitakuwa kwenye makundi manne kama yanavyoonekana hapo chini.

Kundi A:
Azam FC (Tanzania Bara),
JKU (Zanzibar),
Kator (Sudan Kusini),
Uga (Uganda).

Kundi B:
Rayon (Rwanda),
Gor Mahia (Kenya),
Ports (Djiboud),
Lydia (Burundi).

Kundi C:
Vipers (Uganda),
Simba SC (Tanzania Bara), 
St. George (Ethiopia),
Dakadaha (Somalia).