Monday , 24th Nov , 2014

Chama cha mchezo wa Gofu nchini TGU,kinatarajia kufanya Uchaguzi Mkuu wa Viongozi mwakani ikiwa ni pamoja kufanya juhudi za kukuza na kuuboresha mchezo huo hapa nchini kwa vijana wenye umri wa miaka sita mpaka 18.

Akizungumza na East Africa Radio,Makamu wa Rais wa TGU,Joseph Tango amesema pamoja na uchaguzi huo,wanatarajia kutafuta timu ya Taifa ya vijana ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mashindano ya Kimataifa yanayotarajiwa kufanyika Aprili Nairobi nchini kenya.

Tango amesema wazazi pia wanatakiwa kuwa na ushirikiano katika suala la kukuza vipaji kwa vijana ikiwa ni pamoja na kuwah\ruhusu wanafunzi kushiriki mashindano mbalimbali katika mchezo huo ili kuweza kupata vijana watakaoweza kuunda timu mbalimbali hapa nchini.