Tuesday , 18th Nov , 2014

Baada ya Ethiopia kujiondoa kuwa mwenyeji wa michuano Soka ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na kati CECAFA mwaka huu, Timu ya Taifa ya Tanzania, taifa Stars imevunja kambi ambayo ilikuwa ni sehemu ya kujiandaa na michuano hiyo.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka nchini TFF, Boniface Wambura amesema kocha Mart Nooij alishaanza maandalizi ya michuano hiyo ambapo timu ilitakiwa kuweka kambi nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo.

Wambura amesema CECAFA itakapotangaza nchi mwenyeji wa michuano hiyo, kocha ataandaa programu kwa ajili ya mandalizi ya michuano hiyo.