Tuesday , 19th Jan , 2016

Chama cha Mpira wa Wavu Mkoa wa Dar es salaam DAREVA kimesema kimeanzisha ligi ya walemavu wakiwa na lengo la kukuza mchezo huu kwa upande wa walemavu.

Mwenyekiti wa kamati ya ufundi ya DAREVA Nassoro Sharrif amesema, mpaka sasa wameandaa timu ambapo jumla wanatimu sita zikiwa nne za wanaume na mbili za wanawake.

Sharrif amesema, wameanza na mkoa wa Dar es salaam lakini hapo baadaye wanatarajia kuhamasisha viongozi wa vyama vya mikoa ili kuweza kupata timu nyingi zaidi za walemavu ambazo zitaweza kuunda timu nyingi kwa hapa nchini.