
Maeneo ambako uwanja huo utajengwa, kushoto ni Mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete
Akizungumza na East Africa Radio, Mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete amesema ujenzi wa uwanja wa kisasa katika jimbo hilo, ni kuboresha miundombinu na kukuza michezo jimboni humo.
Ufadhili wa ujenzi wa uwanja huo wa michezo kwa watoto wa Msoga ni muendelezo wa ufadhili wa China katika kijiji cha Msoga baada ya kujenga shule ya msingi Msoga.