CAF imetangaza orodha ya wachezaji 21 kwa kila nchi mshiriki zinazoshiiriki mashindano hayo yatakayoanza Mei 14-28 nchini Gabon, huku timu nne za juu zikipata nafasi ya kushiriki Fainali za Kombe la Dunia baadae mwaka huu nchini India.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika {CAF} leo limetoa orodha ya wachezaji 21 watakaocheza Fainali za vijana chini ya miaka 17 (U17) zinazotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwishoni mwa juma hili huko nchini Gabon.