
Shirikisho la soka barani CAF limeiondoa Entente Setif kufuatia utovu wa nidhamu wa mashabiki wa timu hiyo ilipokuwa ikichuana dhidi ya klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Mechi hiyo ya tarehe 18 Juni ilisimamishwa na muamuzi baada ya ghasia kuibuka miongoni mwa mashabiki wa timu hizo mbili.
Mechi hiyo iliposimamishwa Sundowns walikuwa wakiongoza kwa mabao 2-0.
CAF imesema kuwa mawe na vitu vingine vilitupwa uwanjani pamoja na fataki na kusababisha mechi hiyo kutibuka na baada ya muda kidogo mashabiki walivamia uwanjani wakipinga matokeo hayo.
Chanzo BBC.