Sunday , 28th Dec , 2014

Chama cha mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es salaam BD, kimesema kimejiandaa kukabiliana na changamoto mbalimbali zitakazojitokeza katika mzunguko wa pili wa Ligi ya Kikapu mkoa wa Dar es salaam RBA inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Junuari 6 mwakani

Akizungumza na East Africa Radio, Makamu wa Rais wa BD, Richard Julles amesema wamefanya mabadiliko makubwa kwa ajili ya kuhakikisha wanapambana na changamoto zilizokuwa zikitatiza ligi katika mzunguko wa Kwanza.

Julles amesema vilabu pia vinajua changamoto zilizokuwepo pamoja na ugumu wa ligi hivyo itawasaidia kuweza kupambana na kuboresha ili kuweza kuiboresha zaidi.