Alizaliwa Oktoba 25, 1975, huko Kongo na kisha wazazi wake kuhamia nchini Afrika Kusini na kuishi huko rasmi, na hatimaye kupata uraia wa Afrika Kusini.
Umaarufu wa Alph Lukau ulivyoanza
Alph Lukau alianza kupata umaarufu mkubwa baada ya kuanzisha kanisa lake la Alleluia Ministry, ambalo lilijizolea umaarufu mkubwa kwa miujiza iliyokuwa ikitolewa na uponyaji wa kushangaza watu.
Katika shughuli zake za kumtumikia Mungu na uponyaji, ambapo alishwahi kuponya mwanamke aliyeletwa kwa gari la wagonjwa, ambaye alikuwa hajiwezi kabisa kutokana na figo zake kufeli na nyonga kuchomoka. Lakini baada ya kumuombea mwanamke huyoa lisimama na kutembea mwenyewe.
Pastor Lukau alishwahi kuonekana akiponya watu wodini, lakini mpaka sasa haijajulikana ni hospitali gani ambayo uponyaji huo ulifanyika.
Hata hivyo mchungaji huyo aliendelea kufanya miujiza mbali mbali kwa watu waliomwamini, hadi hivi karibuni alipotikisa Afrika na dunia baada ya kusambaa kwa video ikimuonesha akimfufua mtu, ambaye baadaye ilikuja kugundulika kuwa mtu huyo hakuwa amekufa kama ilivyoelezwa.
Pastor Lukau ambaye ameoa na ana watoto pia, anamiliki majumba, magari ya kifahari na ndege binafsi, huku akitajwa kuwa na utajiri wa dola billioni moja. Ni miongoni mwa watumishi wa Mungu weye pesa nyingi zaidi duniani, huku kanisa lake likiendelea kuingiza maelfu ya watu.
Sehemu ya mali anazomiliki Mchungaji Lukau
Licha ya hayo Pastor Lukau amekuwa akiishi maisha ya kifahari kama kupanda ndege mara kwa mara, kutembea na msafara wa magari na wasindikizaji kibao, huku kukiwa na farasi pembeni na magari ya ving'ola.
Hayo ndio maisha ya mchungaji Alph Lukau wa Afrika Kusini kwa ufupi, ambaye amepata umaarufu zaidi baada ya habari za kumfufua mtu.