Wednesday , 1st Apr , 2015

Mume wa msanii na mfanyabiashara maarufu nchini Uganda Zari Hassan, Ivan Semwanga imeelezwa kuwa kutokana na kutoelewana na mama watoto wake huyo, hivi sasa naye ameamua kuanza mahusiano na mwanadada anayejulikana kwa jina la Malkia wa kichaga.

Msanii wa muziki na mfanyabiashara maarufu nchini Uganda Zari Hassan

Aidha, Zari alimkandia mwanadada huyo maarufu kama Malkia wa kichaga kuwa amekwama nchini Marekani na hawezi kusafiri kuja barani Afrika kutokana na kuishi Marekani kwa kutumia nyaraka zisizo rasmi.

Kumekuwa na uvumi juu ya ujauzito wa mwanadada Zari kutokana na mama watoto huyo wa Ivan kuanza mahusiano na nyota Diamond Platinumz, ambapo hata hivyo mwanadada huyo alielezea kupitia mtandao kuwa si ujauzito wa Diamond.