Thursday , 23rd Jun , 2016

Baada ya mengi kutokea na kuvuma juu ya tetesi za utumizi wa madawa ya kulevya kwa msanii wa bongo fleva Young D hatimaye amerudi tena kwa kiongozi wake wa zamani Max na kutangaza kuacha ngada mbele ya waandishi wa habari.

Young Dee akiwa na Max.

Enewz imezungumza na MAX na tukamuuliza tulitegemea kusikia wimbo mpya wa Young D leo hii na alikuwa, je nini kinaendelea.. Max alijibu kuwa msanii huyo yupo katika hatua za mwisho kabisa katika kuandaa wimbo wake mpya.

Hata hivyo amesema kuhusiana na swala la utumiaji wa madawa ya kulevya walimpeleka Young D 'rehab' na waliambiwa kuwa kwa hali aliyo nayo kwa sasa anaweza kuondoka naye kwa kuwa hajafikia hatua mbaya na amekubali mwenyewe kuacha.

Vilevile Max amesema waliambiwa na madaktari wa 'Rehab' kwamba Young D akiacha kutumia madawa atakuwa anakula sana hali ambayo wanaiona sasa kwa msanii huyo na kusema kwamba Young D kwa sasa amebadilika na ana nidhamu kwa watu wote tofauti na awali.