Friday , 3rd Oct , 2014

Rapa Xtatic kutoka nchini Kenya, ametangaza rasmi timu mpya itakayokuwa inasimamia kazi zake za muziki, Broadview Corporation ambapo ameamua kuachana na Rockstar 4000 waliokuwa wanamfanyia kazi hiyo.

rapa wa kike nchini Kenya Xstatic

Xtatic amesema kuwa, uamuzi huo haumaanishi kuwa amepoteza mkataba wake mkubwa na kampuni ya kimataifa kutoka Afrika Kusini ambayo inaendesha kazi zake katika wigo wa kimataifa.

Kwa mujibu wa maelezo aliyotoa kupitia ukurasa wake wa Facebook hivi karibuni, Xtatic amesema kuwa anautambua mchango wa Rockstar katika kila walichomfanyia ila kwa sasa anaona ni wakati muafaka kuendelea na mambo mengine.