Saturday , 31st Oct , 2015

Msanii mkali toka NIGERIA WIZKID ametua jijini Dar es salaam usiku wa jana tayari kabisa kwa kutoa burudani ya LIVE yenye kiwango cha kimataifa akiwa na band yake katika onyesho la #WizkidLiveInDar Leaders Club usiku wa leo.

Dj Snype | Sam Misago (East Africa Radio/TV) | Wizkid

Katika mahojiano ya awali kabisa na eNewz staa huyo ameelezea namna ambavyo anawakubali na kuwapenda mashabiki wake kutoka Tazania, akiwa ametua kwa lengo moja tu la kukata kiu yao ya muda mrefu ya burudani kutoka kwake, akiweka bayana kuwa watoto wa kike wajitokeze kwa wingi kutokana na kuwakubali kwa aina yake.

Star huyo mchana wa leo ameweza kutua katika studio za East Africa Radio ambapo mbali na kuahidi kutoa show nzuri, ameweza kuzungumza mambo mengi ikiwepo heshima aliyonayo kwa wasanii wenzake kiasi cha kuogopa kushindanishwa, binafsi akieleza kuwa amejikita katika kufanya muziki mzuri tu.

Akiwa na Hits zinazofikia 50, Wizkid ameeleza kuwa anajizikia baraka kuweza kuuzunguka ulimwengu kuburudisha mashabiki wake, na kupokelewa vyema katika jukwaa la kimataifa, kuweza kufanya kazi na wasanii wakubwa akiwepo Chris Brown, Tyga, Drake, Ty Dollar $ign, Rihanna, R Kelly na wengine wengi.

Pembeni ya mambo yote, shughuli nzima ni pale Leaders Club kuanzia jioni ya leo ambapo unapata nafasi ya kumshuhudia star huyu aki 'Perform' LIVE kwa mara ya kwanza Tanzania kwa kiingilio cha elfu 20 pekee kawaida na 10000 VIP huku akipewa shavu na Diamond, Fid Q bila kumsahau Christian Bella.. Njoo tufurahi pamoja

Muda ndio huo umefika... Sogea sasa viwanja vya Leaders Club kushuhudia show ya LIVE ya WIZKID ‪#‎WizkidLiveInDar‬