Tuesday , 30th Jun , 2015

Baada ya kumsikia Witnesz jana katika kipindi cha Planet Bongo akikanusha juu ya uvumi kuwa hawezi kupata mtoto tena, staa huyo pamoja na mpenzi wake Ochu Sheggy wamefunguka juu ya ndoa yao hiyo.

msanii wa muziki wa bongofleva Witnesz akiwa na mchumba wake Ochu Sheggy

Witnesz amesema kuwa, kwa muda waliokaa pamoja mpaka sasa, kisheria wao ni kama mume na mke.

Diva huyo mkali wa michano ameeleza pia, kuhusiana na tukio la kufunga ndoa lenyewe linalotambulika kijamii, bado anamsubiri mumewe Ochu kuchukua hatua hiyo kutokana na kuwa yeye ndio muoaji.