Tuesday , 29th Nov , 2016

Waziri wa Habari Sanaa na Michezo, Mh, Nape Moses Nnauye, amesema ana imani na tuzo za EATV, kuwa zitaleta hamasa na changamoto kubwa kwenye tasnia ya sanaa.

Waziri Nape Nnauye

Akizungumza na eNewz ya EATV, Waziri Nape amesema yeye binafsi aliyapitia majina ya wasanii waliofanikiwa kuingia kwenye tuzo hizo na kusema ni wasanii wazuri na waliostahili, hivyo anaamini EATV itatenda haki kwa kutoa tuzo kwa yule aliyestahili kupewa.

"Nilisoma yale majina mliyoyaweka, yataleta ushindani mkubwa sana tu, kwa sababu walichaguliwa watu wazuri, na mimi nadhani watanzania watatumia fursa hiyo kupiga kura na kuonesha mapenzi yao, na naamini East Africa TV watatenda haki kumpata mshindi wa kweli kutokana na ubora wa kazi yake", alisema Waziri Nape.

Waziri Nape pia alitumia fursa hiyo kuipongeza EATV kwa kuanzisha tuzo,  kwani itakuwa chachu katika kuibua vipaji vipya na kukuza sanaa ya Afrika Mashariki.

"Mimi nawapongeza sana kwa sababu kupitia tuzo kama hizi ndipo ambapo tutaibua vipaji, tutawahamasisha washindane kwa ubora sio kwa vioja",

Mtazame hapa akizungumzia EATV AWARDS

https://youtu.be/4xo02G1lhlw

Tags: