
Msanii Witness
Akizungumza na EATV kuhusu namna alivyoona mashindano ya Dance100% ambapo yeye alishiriki kama Jaji mwalikwa wa hatua ya nusu fainali, Witness amesema mashindano ni mazuri ila wasichana wanaonekana kuogopa mazoezi na kujiunga na makundi ndiyo maana hadi hatua ya nusu fainali yupo binti mmoja tu.
“Kutokana na wasichana wengi kujitokeza nashauri pengine kama wasichana wakirshiriki kivyao na wavulana kivyao waje kukutana hatua ya fainali jambo hilo linaweza kusaidia kuongeza idadi ya wasichana watakaoshiriki” Amesema Witness.
Aidha msanii huyo amewataka wasichana kuchangamkia nafasi za bure zinazojitokeza ili waweze kuonesha vipaji vyao na kwa kufanya hivyo wanaweza kutambulika ndani ya jamii yetu na nje ya nchi pia.
Shindano la Dance100% linaoneshwa na EATV pekee kila Jumapili saa moja jioni na kudhaminiwa na kinywaji baridi cha Coca Cola na