
Kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii, wasanii hao wamendika jumbe mbali mbali wakionyesha kufurahia uhuru wa wasanii wenzao hao, ambao walifungwa kwa muda mrefu kutokana na makosa yaliyokuwa yanawakabili.
Baadhi ya wasanii hao ni Roma Mkatoliki aliyeandika 'Welcome Home #Fam #Papii #Nguza#Mungu-ni-mwema, Aslay Isihaka ameandika Muda Umejibu Asante Mh Rais Kwa Hili, Billnas nae alipost picha ya Babu seya na mwanae na kuandika 'heri ya sikuu yetu ya Uhuru'.
Nguza na wanawe watatu walikamatwa Oktoba 12 mwaka 2003 na walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Oktoba 16, mwaka 2003, wakituhumiwa kubaka na kunajisi watoto 10, na Juni 25, 2004 Mahakama iliwatia hatiani na kuwahukumu kwenda jela maisha kwenye Gereza la Ukonga, Dar es Salaam.
