
Mbunge wa Jimbo la Mikumi ambaye pia ni mwanamuziki wa Hip hop, Joseph Haule
Prof. Jay amebainisha hayo muda mchache alipotoka katika kikao cha Bunge na kusema serikali inapaswa kuzingatia kilio hicho cha wasanii kwa kusimamia kuwepo kwa hati miliki ili kuweza kuongeza pato la taifa kupitia kazi za wasanii.
“Kilio kikubwa cha wasanii wa Tanzania sasa hivi ni kuhusu masuala yao ya hati miliki na ukiangalia Sheria ya hati miliki namba 7 ya mwaka 1999 imeonekana kuwa na mapungufu makubwa sana, kiasi kwamba wasanii watanzania hawapati kile kinachostahili, hawapati jasho lao linavyotakiwa na wasanii wa Tanzania wamekata tama lakini kiukweli kabisa takwimu na tafiti zilizofanywa na ‘Lulu Art Promoters’ inaonyesha kwamba wasanii wa Tanzania na sanaa ya muziki pekee yake inachangia zaidi ya asilimia 1 ya pato la taifa”. Alisema Mbunge huyo
Aidha, Prof. Jay aliendelea kwa kusisitiza kwamba “Muziki ni nyanja muhimu sana, kiukweli ikitupiwa jicho na kuweza kupewa kipaumbele wasanii wanaweza wakupata kile kinachostahili ili kuongeza pato kubwa katika taifa letu.” Alisisitiza Prof. Jay