Chin Bees amesema hayo kupitia eNewz ya EATV na kusema kitendo hicho kinamnyong'onyesha sana kuona baadhi ya watu wanaweza kufaidika kimaisha kupitia vipaji vya wenzao na kushindwa hata kuwathamini wahusika wanaojitoa kwenye suala la uandishi.
“Siwaandikii kutokana na watu wanachukulia poa unajua…Sasa hivi mtu akija labda akubaliane na ‘price’ yangu nitakayo mtajia kwamba kiasi flani kazi, ukishindwa kumudu ‘over’ hiyo ndiyo kitu naweza kukifanya kwasababu watu hawana 'respect' unajua, watu wanapata maisha kupitia ‘talent’ za watu lakini bado sisi tunabaki si unajua vile”- Alisema Chin Bees.
Mtazame hapa chini akifunguka kwa undani zaidi
