Kamikaze ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa tofauti na watu wengi walivyokariri, kwamba muziki wa sasa hivi ukiwa na video nzuri ndio unafanikiwa.
“Unaweza ukawa na video kali alafu usihiti, muziki ni zaidi ya chupa kali, ukirudhisha miaka flan nyuma ngoma kali ndio ilikuwa inahit, lakini sasa msanii akitaka kupigwa na radio atataka kitu flan, hivyp muziki ni zaidi ya ngoma kali zaidi ya chupa kali”, alisema Kamikaze.
Pamoja na hayo Kamikaze ameongelea kuhusu kurudi kwa kundi lao la Wakacha, ambalo msanii mwenzake wa kundi hilo Juma Jux alisema litarudi hivi karibuni; kwa kuwa walijikita kwenye muziki wa solo.
“Wakacha ipo tunajua tuna lawama nyingi kwa mashabiki, lakini Jux yupo wote tulikuwa tunafanya kwanza kama solo artist, lakini sasa hivi tunalirudisha na wote tupo”, alisema Kamikaze.
Pia msanii Kamikaze ameongelea mipango yake ya mwakani akisema ana mpango wa kutoa albam mbili, kwani msanii bila kutoa albam ni kitu ambacho hakiwezekani.
“Nina albam mbili ambazo zitatoka mwakani, baada ya miezi miwili au mitatu nitatoa wimbo ambao utakaribisha albam, unajua passpot ya msaniii kokote kule lazima uwe na albam, iwe utauza au hujauza lakini jukumu lako limekamilika kama msanii”, alisema Kamikaze.