Akizungumza katika uzinduzi huu, Meneja Masoko wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe amesema kuwa mchakato wa tuzo hizi kwa mwaka huu utahusisha watu wote kuanzia hatua ya awali ya kupendekeza wasanii watakaowania tuzo.
Vilevile Mratibu wa Tuzo hizo za za Muziki Tanzania kwa mwaka 2014 kutoka Basata , Kurwijira Maregesi, amesema kuwa vipengele vya kuwania tuzo kwa mwaka huu vitakuwa 36, ambapo pia kuna mabadiliko kadhaa katika baadhi ya vipengele kwa ajili ya kuboresha zaidi tuzo hizo.
Mwaka 2013 kulikua na category 37 ambapo Mwaka huu imeondolewa moja kutokana na maoni mbalimbali ya wadau wa muziki ambapo category yenyewe ni Mtayarishaji chipukizi wa mwaka.
Category zilizobadilishwa majina mwaka huu 2014 ni Mtumbuizaji bora wa kike wa muziki badala ya msanii bora wa kike ilivyokua mwaka jana, mtumbuizaji bora wa kiume wa muziki badala ya msanii bora wa kiume mwaka jana, mwimbaji bora wa kiume Taarab ambayo mwaka jana ilikua msanii bora wa kiume Taarab.
Mwimbaji bora wa kiume bongofleva badala ya mwaka jana Msanii bora wa kiume bongofleva, mwimbaji bora kiume band ambayo mwaka jana ilikua msanii bora wa kiume band, mwimbaji bora wa kike bongofleva badala ya mwaka jana msanii bora wa kike bongofleva.
Mwimbaji bora wa kike Taarab badala ya mwaka jana msanii bora wa kike Taarab, mwimbaji bora wa kike band badala ya msanii bora wa kike band.
Kwa mujibu wa Baraza la sanaa la Taifa, mabadiliko yaliyofanywa kwenye tuzo za mwaka huu wa 2014 ni kutokana na maoni na mapendekezo ya wadau wa tasnia ya muziki kutoa sababu mbalimbali.