Friday , 26th Jun , 2015

Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Joseph Mbilinyi leo hii amejibu tuhuma nzito bungeni, zilizotolewa juu yake na mbunge mwenzake, Mhe. Martha Mlata aliyemlaumu kutumia mabavu dhidi mzazi mwenzake Faiza Ally kwa kumnyanganya mtoto wao kwa amri ya mahakama.

Mhe. Joseph Mbilinyi

Mhe. Mbilinyi maarufu zaidi kama Sugu amesisitiza kuwa, suala hilo kwa mtu yoyote mwenye akili timamu angependa libaki kuwa binafsi, akijitetea kutimiza huduma za malezi ya mtoto akiwa kama baba kipindi mtoto analelewa na Faiza, na kufuata taratibu kisheria kumchukua mtoto huyo kutokana na hofu ya maadili ya mama yake kama anavyoeleza hapa.