Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Stamina afungukia kulainisha mashairi

Saturday , 27th May , 2017

Rappa Stamina anaye-hit kwa sasa na ngoma ya 'Love Me' amefunguka na kudai ameamua kuimba wimbo wa mapenzi, siyo kwa sababu nyimbo zake ngumu zimebuma bali amebadilika kidogo ili kuimba vitu vilivyopo kwenye jamii kwa kuwa yeye ni msanii.

Stamina

Stamina amefunguka hayo mbele ya kamera za eNewz na kudai kwamba ujio wake mpya ameamua kuimba maisha yaliyopo kwenye jamii inayomzunguka na kuongeza kuwa hajatoa kwa sababu ameumizwa kimapenzi bali yeye kama msanii ni wajibu wake kwa kuwa mapenzi ni maisha yaliyopo kwenye sehemu jamii.

Akizungumza kuhusu kuimba mapenzi kitu ambacho siyo kawaida yake, Stamina amesema "Hakuna kitu kigumu mbele ya mapenzi kwani hata wana hip hop tuna hisia kama watu wengine. Sijatoa 'Love me' kwa sababu nimetendwa ila nimeimba kuwasilisha kazi ya sanaa kwa sababu mimi ni msanii. Mwana hip hop akitoa nyimbo ya mapenzi watu wanamshangaa kwani sisi ndio hatuna wapenzi? mapenzi ni sehemu ya maisha" Stamina alifunguka.

Kwa upande mwingine rappa huyo ambaye amemshirikisha  Maua Sama  katika wimbo wake mpya amefunguka na kusema kwamba hakuna wimbo wowote duniani unaobuma kwenye game bali mapokezi ndiyo husababisha kazi kuwa hit au kuonekana kawaida.

"Hakunaga ngoma inayobuma duniani, kwa sababu ngoma wewe unayohisi imebuma kwako kwa mtu mwingine ni kali sana na kwenye simu yake utakuta ndiyo anaisikiliza sana. Ila kinachotokea ni ngoma kushindwa kufika mahali palipotarajiwa na wakati mwingine siyo lazima zote zifike. Kitu kama hit inatokeaga tu kutokana na mapokezi ya watu' Stamina aliongeza.

Fungua link hapa chini kumtazama Stamina alivyofunguka.
 

HABARI ZAIDI

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea

Bashiri Mohamed (35) Mwenye Koti Jeusi akiwa anafikishwa Mahakamani Ilemela, Jijini Mwanza

Aliyezini na binti yake apandishwa kizimbani