Belle 9 akiwa Kikaangoni leo
Belle 9 alisema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Kikaangoni kinachofanyika kupitia ukurasa wa facebook wa EATV kila Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi jioni.
"Mimi ni shabiki mzuri wa Yanga hivyo chama langu ni Yanga, siwezi kuhama chama langu kisa matokeo ya jana dhidi ya Simba kila mtu aliona jinsi mchezo ulivyochezwa dakika tisini hivyo yale ni matokeo tu , siwezi kuhama Yanga' alisisitiza Belle 9
Mbali na hilo Belle 9 amesema moja ya mipango yake ni kuhakikisha anakuwa na band yake mwenyewe na kuanza kufanya muziki wa 'live' ili akamilike kabisa kuwa mwanamuziki kwa kujifunza vitu mbalimbali katika muziki.