Thursday , 15th Nov , 2018

Msanii wa Bongofleva Billnass baada ya kumchunia Nandy wakati anajaribu kuimba nae katika tamasha la  kutambulisha album yake ya 'African Princes' hivi karibuni, amesema hakuwa tayari kuimba.

Wasanii Nandy na Billnass

Akiongea kupitia eNEWZ Billnass amesema sio kila sehemu anakuwa kama msanii, kuna sehemu nyingine anatokea kama mtu wa kawaida tu na sio mara zote anakuwa tayari kuimba na sio lazima kila anakokwenda afanye shughuli na kushiriki kama msanii.

Billnass aliendelea kusema kwamba "Sapoti niliyotoa ya kununua album na kufika pale inatosha, sioni sababu ya kuendeleza uadui baina yangu na Nandy mimi pale nilienda kumpa sapoti yangu kama msanii mwezangu na si vinginevyo, hivyo alivyonipa Mic kwa kweli sikujua alitaka nifanye nini kwa wakati ule kwa kuwa sikuwa tayari kabisa kwa kuimba".

Hata hivyo Billnass alisema ni miezi 4 sasa tangu ameachia wimbo wake wa mwisho hivyo kazi mpya inakuja siku sio nyingi na anachoamini ni kwamba hajawahi kufeli katika kazi zake hivyo hata ujio wake mpya utafanya vizuri kama ilivyo kawaida yake kutengeneza nyimbo zinazotengeneza misemo katika jamii.