Monday , 30th Mar , 2015

Wasanii wanaounda kundi maarufu la muziki la Sauti Sol la nchini Kenya baada ya kufanya vyema kujitangaza kimataifa hivi sasa wamejiandaa kufanya project kubwa na kundi nyota la nchini Afrika Kusini, Mi casa.

wasanii wa kundi maarufu la Sauti Sol nchini Kenya

Sauti Sol ambao rekodi yao inayoendelea kutamba hivi sasa ya 'Sura Yako' wameelezea kuwa project hii wameibatiza jina #Solgenereation #Africanshine.

Hii ni moja ya hatua yao kubwa ambayo kundi hilo limeamua kuanza kuungana na wasanii hao wa nchini Afrika Kusini na wamewasihi mashabiki kuwa kazi hiyo itaanza muda wowote kuanzia sasa.