Sunday , 1st Jun , 2014

Msanii anayeongoza bendi maarufu ya walemavu inayoitwa 'Tunaweza Band' Ras 6 hivi sasa anakusanya nguvu zake katika muziki ambapo anatarajia kutoa singo yake mpya iliyobatizwa jina 'NO' ambayo inatarajia kutoka mwanzoni mwa mwezi huu wa Sita.

Ras 6 ameongea na eNewz kuwa nyimbo hiyo mpya inaongelea wanandoa ambao ni mafukara waliobahatika kupewa fedha nyingi na tajiri, ili wamuuzie tajiri huyo mtoto wao mwenye ulemavu kwa kumtoa kafara ili kustawisha biashara zake, sehemu nyingine inahusu wanamgambo wanavyonyanyasa wamachinga.

Ras 6 amesema kuwa atatoa audio kwanza kisha itafuatiwa na video hivyo mashabiki wakae mkao wa kula.