Friday , 28th Aug , 2015

Rapa Octopizzo wa nchini Kenya, anakabiliwa na kibarua cha kujitetea kwa mashabiki wake juu ya mustakabali wa ngoma yake ya 'This Could Be Us' aliyodai kumshirikisha star kutoka Marekani, August Alsina.

Rapa Octopizzo wa nchini Kenya

Hii ni baada ya uongozi wa msanii huyo wa kimataifa kukana Agust kuhusika katika kazi hiyo.

Maswali mengi yalizuka baada ya video ya kazi hiyo kutoka bila August kuonekana ndani yake, kitu ambacho kiliwaudhi mashabiki wengi, na mpaka sasa marekebisho yamekwishafanyika mtandaoni kuondoa jina la msanii huyo katika kazi yenyewe.

Kitendo cha kufanyika kwa marekebisho hayo na Octopizzo kutokupatikana kutolea ufafanuzi suala hilo kunaacha jibu moja tu kwa mashabiki wa muziki kuwa hiyo ni mbinu tu ambayo aliamua kuitumia kuipatia kiki rekodi yake hiyo mpya kutoka albam yake ya LDPC anayoitangaza sasa.