Wednesday , 18th Mar , 2015

Rapa Octopizzo kutoka nchini Kenya, ameingia katika harakati mpya za kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa kike, kupitia kampeni zinazofahamika kwa jina Violence Against Women and Girls.

msanii wa miondoko ya Hip Hop nchini Kenya Octopizzo

Kupitia kampeni hizo, Octopizzo tayari amekwishashiriki kuandaa mashindano yenye lengo la kukutanisha pamoja umati wa watu na kuwafikishia ujumbe huo, kuhusu kuepusha vitendo vya uonevu, udhalilishaji na ukatili dhidi ya jinsia ya kike.

Kampeni hizo zina lengo la kutokomeza kabisa vitendo vya kushambulia wanawake na kuwapiga, kuwadhalilisha kijinsia na mambo mengine yanayofanana na hilo katika jamii ya Kenya.