Wednesday , 6th Jan , 2016

Mahakama Kuu kupitia Mheshimiwa Jaji IGNAS KITUTSI asubuhi ya leo imetupilia mbali maombi madogo ya kesi ya kuomba kupunguziwa gharama za dhamana ya kesi iliyofunguliwa na mwanasiasa Jonas Nkya dhidi ya msanii/mbunge Joseph Haule (Profesa Jay).

Professa Jay na Wakili wake Tundu Lissu

Mahakama imetupilia mbali kesi hiyo na kukubaliana na hoja za mapingamizi ya kisheria yaliyowekwa na jopo la mawakili wa msanii huyo - Tundu Lissu na John Mallya.

Mahakama pia imemuamuru mlalamikaji Jonas Nkya ambaye walikuwa wakigombea pamoja nafasi ya ubunge wa jimbo la Mikumi alipe gharama zote za kesi na usumbufu.