Thursday , 18th Sep , 2014

Kutoka nchini Kenya, Rapa Octopizzo ameendelea na shughuli zake za hisani kutembelea kambi za wakimbizi kufundisha, kuhamasisha na kuwajenga vijana katika kambi hizo hususan katika nyanja za sanaa hususan muziki pamoja na michezo.

rapa wa nchini Kenya Octopizzo

Safari hii rapa huyu ameweza kufika katika kambi maarufu ya Daadab na kutumia muda wa kutosha kukaa na vijana kwa ajili ya shughuli hii, akiwa kama moja ya wasanii wenye ushawishi mkubwa kwa vijana kundi hilo ndani na nje ya mipaka ya Kenya.

Mapema mwezi Juni rapa huyu alipata nafasi pia ya kufika katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma kwa ajili ya shughuli kama hii, ambapo ameeleza kuwa amekuwa akijifunza mambo mbali mbali kuhusiana na maisha kupitia ziara zake hizi.