Friday , 25th Jul , 2014

Rapa Octopizzo, ameweka wazi kuwa, alikuwa na ndoto ya muda kuwa na mahusiano na mama wa mtoto wake Zara, na malengo na kujiamini ndicho kitu kilichomsaidia kumpata.

msanii Octopizzo wa nchini Kenya

Octopizzo kwa njia ya mtandao amesema kuwa, kwa mara ya kwanza alimuona mrembo huyu katika Tangazo kama "model", na tangu hapo alijipanga vyema hadi kumpata.

Rapa huyu kwa sasa anaendesha maisha yake sambamba na mrembo huyu, huku pia akiwa na binti mwingine ambaye anakwenda kwa jina Tracy kutoka kwa mama mwingine.