Monday , 1st Feb , 2016

Octopizzo, rapper kutoka Kenya amesusia kuchukua tuzo aliyoshinda katika tuzo za Bigwa akidai imeshusha hadhi ya kazi zake, kipengele alichoshinda cha 'Comeback Artist Of The Year'.

Octopizzo

Kipengele hicho kimeonesha kumuudhi kutokana na imani yake binafsi kuwa amekuwa muda wote kwenye game bila kuachia nafasi toka alipoanza.

Rapper huyu amesema kuwa amekuwa akifanya kazi kwa bidii hata kushinda wasanii wengine wa hip hop nchini Kenya, kitendo cha kupewa tuzo ya msanii aliye rejea wa mwaka kikiwa ni kama utani kwake.

Kupitia maelezo yake ya kina, Octopizzo amesema kuwa waratibu wa tuzo wanaweza kumpatia msanii Wahu aliyekuwa anawania naye kipengele hicho, kauli ambayo imeonekana kumuudhi Nameless ambaye ni mume wa msanii huyo, akimtaka rapa huyo kuheshimu kila tuzo akifahamu kuwa itafika mahali kazi zake hazitatambuliwa tena na mtu yoyote.

Nameless amekazia ujumbe wake huo na neno kuntu kwa Octopizzo.. Tuheshimiane.