Wednesday , 7th Oct , 2015

Rapa Nonini kwa kushirikiana na mastaa wenzake kupitia taasisi yao ya hisani ya Entertainment With Fun for Charity, wamefanikiwa kuchangia magodoro kwa kituo cha watoto huko Kayole, kuondoa tatizo lililokuwa linawakabili la kulala chini.

staa wa muziki wa nchini Kenya Nonini

Kutokana na jitihada za nguvu za msanii huyo akishirikiana na taasisi mbalimbali, kituo hicho kimegaiwa magodoro 20 ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa shughuli za hisani anazoendesha staa huyo pembeni ya muziki, kusaidia jamii hususan watu wale ambao wanaishi katika mazingira magumu.

Wakati huo huo staa huyo amejipanga kwa ajili ya kupeleka kampeni yake ya kusaidia walemavu wa ngozi ya Color Kwa Face huko Mombasa, ambapo wikiendi hii kutafanyika tamasha kuwezesha kupatikana kwa pesa zitakazoingizwa kuendesha shughuli za kampeni hiyo.

Nonini pia kwa sasa anajipanga kwa ajili ya kuachia project yake kubwa kabisa ya muziki aliyomshirikisha star wa muziki Chegge kutoka hapa Tanzania, kazi ambayo itasimama kwa jina 'Wanajishuku'.