Akiongea kwenye kipindi cha Planet bongo Akili The Brain alidai kuwa alizama sana kimapenzi kwa huyu mwanamke kiasi cha kushindwa kufanya mambo mengi na kupelekea mambo yake kukwama kabisa.
"Nilioa mke wa pili nilizama kwenye mapenzi yake kiasi kwamba nilikuwa hata sijielewi, mwanamke yule alikuwa hapendi mimi nifanye muziki kabisa lakini baada ya kuja kuachana naye ndiyo nikaanza kurudi kwenye muziki kwa kuachia kazi moja moja. Nilipokuwa na yule mwanamke hata mimi sijui nilikuwaje yaani naona kama nilikuwa nimelala hivi lakini nashukuru Mungu nilipoachana naye ni kama nimeamka saizi. Saizi nimekoma siwezi kurudia tena kuoa mke wa pili" alisema Akili The Brain
Mbali na hilo Akili The Brain amedai kwa sasa anafanya mpango wa kurudi kwenye muziki na kuachia albam yake kwani ameshatayarisha albam yenye nyimbo zaidi ya kumi.