Saturday , 24th Oct , 2015

Siku hii ya leo ambapo kampeni za vyama vya siasa zinafikia mwisho kuelekea siku ya Uchaguzi Kesh

Nikki Wa Pilli

Siku hii ya leo ambapo kampeni za vyama vya siasa zinafikia mwisho kuelekea siku ya Uchaguzi Kesho, Msomi, Mchambuzi na Rapa Nikki wa Pili kutoka kundi la Weusi ametoa tathmini ya jumla ya mchakato mzima wa kampeni hizo na kueleza kufurahishwa na kuhamasika kwa watu huku kukiwa na tofauti kubwa kati ya ushindani na ubora wa kampeni hizo.

Kwa mujibu wa tathmini ya rapa huyo, ni wazi kuwa watu wengi wanataka mabadiliko ambayo yanahubiriwa na vyama vyote, lakini pande zote mbili, wananchi pamoja na wanasiasa hawajaweza kufanya uchambuzi wa kitu gani hasa wanachotaka kubadili kama ambavyo anaeleza mwenyewe hapa.