Saturday , 11th Jul , 2015

Mwanamuziki wa kimataifa kutoka Ujerumani ambaye anatumia tarumbeta, Mathias Beckmann ametua nchini Tanzania kwa ajili ya kuweza kushirikiana na wanamuziki wa Bongo Flava katika kuchangia ladha na kuupeleka kimataifa zaidi.

Mwamuziki wa Kimataifa kutoka Ujerumani ambaye anatumia trumpt Matthias Beckmann.

Beckmann amesema amevutiwa na mtindo unaotumiwa na wanamuziki wa Tanzania ukichanganya na muziki anaofanya yeye nchini Ujerumani unaweza kuleta ladha tofauti ambayo italeta ladha ya muziki mzuri.

Amesema mpaka sasa anafanya mawasiliano na wanamuziki wa Bongo akiwemo Barnaba, ili kuanza kujaribu kutengeneza muziki huo.