
Isha Mashauzi
Isha Mashauzi ameyasema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio ambapo alikuwa akiwahamasisha wanawake na mabinti wenye uwezo ili kuweza kuwasaidia watoto wa kike waliopo mashuleni waweze kupata pad za kujistiri, kupitia kampeni ya 'Namthamini' inayoendeshwa na East Africa Television LTD wakishirikiana na taasisi ya Haki za Wanawake (HAWA).
Isha Mashauzi amesema wanawake siyo kama hawapendani bali muda mwingine wanakosa hamasa na namna nzuri ya kushirikishwa lakini anakiri wazi kuwa wanawake wanapendana na kusaidiana.
"Unajua sisi wanawake si kama hatupendani sema kuna wakati tunashindwa kusaidiana sababu tu tumekosa hamasa na njia nzuri ya kusaidiana lakini tunashukuru kwa hili linalofanywa na EATV kwani litasaidia wasichana kupata vifaa muhimu katika zile siku zao na kuwafanya kuwa huru na kuhudhuria vyema shule". Alisema Isha Mashauzi
Mbali na hilo Isha Mashauzi alitoa rai kwa watoto wa kike kuendelea kupendana na kujaliana ikiwa pamoja na kuthaminiana