Tuesday , 11th Aug , 2015

Marehemu Sophie Baguma Munobi, mama mzazi wa wasanii Vampino, Sabasaba na Maurice Kirya siku ya leo amefanyiwa ibada ya mwisho huko katika kanisa la St James, Makindye Kampala nchini Uganda.

Staa wa muziki Maurice Kirya akiwa na marehemu mama yake Sophie Baguma Munobi

Ibada hiyo ambayo imekutanisha watu na mastaa mbalimbali katika kanisa hilo imemalizika na kupangwa tayari kwa ajili ya kusafirishwa huko Rwenkoole/Bwijanga kwa ajili ya shughuli ya maziko siku ya Kesho.

Akiongea na eNewz kuhusiana na ratiba ya hiyo ya msiba, Moja ya watoto wa marehemu, staa wa muziki Vampino ameshukuru wote waliokuwa wakimuombea mama yao, akieleza kuwa anaamini kuwa anapumzika sasa baada ya kuusumbuliwa na kansa kwa miaka 5 sasa.