Wednesday , 1st Jul , 2015

Muigizaji filamu Lupita Nyong'o ametajwa kuwa balozi wa kimataifa wa tembo, baada ya kuonekana kwa mara ya kwanza jana nchini Kenya tangu ashinde tuzo ya Oscar.

muigizaji nyota wa Oscar kutoka nchini Kenya Lupita Nyong'o

Ziara yake hiyo ni ya kwanza kwa muigizaji huyo katika nchi ya wazazi wake, baada ya kushinda tuzo hiyo ya juu kutokana na uhusika wake kwenye filamu ya 12 Years a Slave.

Akiongea mbele ya vyombo vya habari Lupita amesema anajivunia kuwa Mkenya na kuwa balozi wa Kimataifa wa kupambana na mauaji ya tembo.