Thursday , 15th May , 2014

Msanii wa muziki wa nchini Kenya, Juliani ameamua kuja kivingine akiwa na ngoma mpya ya kimapenzi ambayo ndani yake anafunguka juu ya mambo mbalimbali ambayo yanahisiwa kuwa ni uhalisia wa hisia zake kutokana na yale ambayo amepitia katika upande huu

Juliani

Kazi hii mpya ya Juliani ni kutoka katika albam yake mpya ya Exponential Potential, na licha ya kuhisiwa kubeba siri juu ya mahusiano ya msanii huyu, pia kazi hii imejaribu kugusia changamoto nyingine mbalimbali katika suala zima la mapenzi.

Kazi hii mpya ya Juliani imepatiwa jina Morio na Juliete ikilinganishwa na kisa maarufu duniani cha wapenzi wawili waliopendana sana Romeo na Juliete.

Tags: