Monday , 24th Mar , 2014

Mwanadada Lupita Nyongo ameendelea kujipatia sifa kubwa kutokana na mafanikio na jina alilojijengea kwa ushiriki wake ndani ya filamu ya 12 Years A Slave, ambapo safari hii ametajwa katika moja ya mashairi ya rapa Jay Z.

Jay Z, Jay Electrica

Mashahiri haya ya Jay Z yanayorusha jina la Lupita Nyong'o ni kutoka katika ngoma inayokwenda kwa jina la We Made It ambayo amefanya pamoja na rapa Jay Electrica, ikiwa ni remix ya ngoma ambayo hapo awali ilifanywa na Soulja Boy.

Kupita eNewz unaweza kusikia kipande cha mstari huu wa Jay Z akimtaja nyota Lupita Nyong'o.