
Young Dee amefunguka hayo wakati akichambua mistari ya Young Killer na Dogo janja na kusema hakasiriki wanavyomuimba bali anaona kama hawajaamua kufanya kazi lakini lakini sasa hawajaamua kufanya kazi bado wapo kwenye vilinge
Kuhusu line ya Dogo Janja iliyopo katika wimbo wake wa ‘My Life’ isemayo, “nyie mayoung hamniwezi’,
"Huu wimbo 'My Life' maana yake maisha yangu, kama naimba wimbo unaohusu maisha yangu siwezi kumzungumzia mtu mwingine, wimbo ni mzuri lakini hiyo part imekuwa kama imetoka nje ya mada. nimekwa nikifuatilia nyimbo kama hizo kwa muda mrefu na sio hiyo tu kuna nyimbo karibia sita na nyingine zipo studio hazijatoka"- alisema Young Dee.
Hata hivyo Rapa huyo anayesimama kama mfalme wa Dar es salaam (anavyojiita) amewataka wasanii hao kuonyesha uwezo wao kwa kufanya kazi na siyo kujisifia wao ni bora kuliko wengine.
Young Dee
“Hata kama wewe ni mkali fanya mambo yako achana na mtu mwingine, simple like that, siwezi kusema mimi ni mkali eti wewe Fid Q huniwezi, hilo hamna kama wewe ni mkali fanya ukali wako. Ni kama shambulio la moja kwa moja lakini huwezi kujua mtu anafanya hiyo kwa lengo gani, mwingine anatafuta publicity, kwa hiyo mimi nitavyoreact ndio itafanya hiyo point ionekane ina make sense au sivyo,” alisema. .
Kuhusu line hiyo Young Dee inayosema ' Kuhusu kufunikwa siwazi, kuhusu janjaro na Young Killer mimi ndio mkubwa wao wa kazi
"Itafika point wataacha hayo mambo na kuamua kufanya kazi, mimi ninapenda kwa sababu wenyewe wanajua kabla hawajatoka mimi ndiye nilikuwa nawapromote, huyo Young Killer nimempigia simu mimi nikiwa na Belle 9 nakamuhamasisha baada ya kumsikia kwenye kipindi cha Fid Friday Free Style, Lakini siwezi kuwajudge kwa sababu ni umri wanaopitia ambao hata mimi nilipitia,” alisema Young Dee.