Tuesday , 6th Jan , 2015

Rapa mkongwe wa bongofleva nchini Inspekta Haroun, amesema kuwa licha ya sanaa yake kupoa tofauti na ilivyokuwa hapo zamani, anaamini kuwa uwezo wake kisanaa bado upo na anaweza kufanya vizuri.

msanii wa bongofleva nchini Inspekta Haroun aka Babu

Inspekta almaarufu kama 'Babu' ameongea na Enewz akisema anaweza kufanya vizuri zaidi na mashabiki kumkubali jukwaani japokuwa kwa muda sasa hajaweza kupata show kubwa ambazo zingeweza kumsimamisha imara.