
amesema kwa sasa hakuna nyimbo kali hata moja kutokana na kutokuwa na vigezo.
Enriko amiambia Planet Bongo ya east Africa Radio kuwa nyimbo nyingi za sasa hivi hazina ubora, hivyo hazikai kwenye chati kwa muda mrefu.
"Mpaka sasa hivi sijaona nyimbo gani ambayo kali, zote naona sawa sawa tu, ni nyimbo ambazo zinaweza kukaa siku mbili tatu wiki tatu wiki nne, nyimbo kali inatakiwa ukae miaka, miaka miwili mitano au sita, wimbo mkali ni jinsi ulivyotungwa, kutokana na mashairi yenyewe yamekuja mazuri, na unaweza ukasema melody yake imekaa vizuri, hata ikikaa sikioni kwa mtu anajua hii nyimbo imeimbwa vizuri, beat zake zimetoka vizuri, vinanda kila kitu vimewekwa sawa sawa", alisema Enriko.