Monday , 15th Dec , 2014

Msanii wa muziki wa nchini Uganda, Mun G amemtangaza rasmi rapa GNL Zamba kuwa ndiye atakayekuwa msimamizi rasmi wa harusi yake ambayo itafanyika hivi karibuni baada ya kukamilika kwa ratiba ya kujitambulisha kwa wakwe mwishoni mwa wiki.

msanii wa muziki wa Uganda Mun G akiwa na mchumba wake Clara

Harusi ya msanii huyu inatarajiwa kuwa tukio jingine kubwa katika ulimwengu wa burudani Uganda ambapo mpaka sasa mashabiki wa msanii huyu wanasubiri kwa hamu kutangazwa kwa tarehe rasmi ya tukio la harusi ya staa huyu.

Mun G ambaye jina lake halisi ni Emmanuel Matovu pamoja na mchumba wake ambaye anafahamika kwa jina Clara, wamekuwa wakiishi pamoja tangu mwanzoni mwa mwaka huu, na sasa msanii huyu ameamua kumaliza mwaka kwa kurasimisha uhusiano wake huo kwa mujibu wa taratibu za kiimani na kiutamaduni.