Thursday , 23rd Jul , 2015

Nuh Mziwanda, ambaye kwa siku kadhaa ameweza kuamsha mjadala mitandaoni kutokana na kile kilichotengenezwa kuonekana kuwa ameachana na mpenzi wake Shilole, na hatimaye sasa kuweka bayana ujio wa kolabo yao mpya.

Wasanii wa muziki ambao ni wapenzi Nuh Mziwanda na Shilole

Nuh ameitambulisha kolabo hiyo inayokwenda kwa jina 'Ganda la Ndizi', ameweka bayana namna mashabiki walivyopokea kile walichokifanya na kile walichojifunza kutokana na kitendo walichofanya.

Nuh ameweka wazi kuwa tukio hilo limemuwezesha kuelewa zaidi vile ambavyo mashabiki wanalichukulia penzi lao kama anavyoeleza hapa, sambamba na hili pia unapata nafasi kidogo ya kusikiliza kolabo hii na Nuh na Shilole, 'Ganda la Ndizi'.