Tuesday , 3rd Nov , 2015

Star wa muziki Frasha kutoka kundi la P-Unit Kenya, amejikita katika kampeni ya kupambana na utumiaji wa pombe ambao umekuwa na athari kwa kiasi kikubwa katika jamii, akiwa binafsi amekamilisha lengo la kukaa siku 40 bila kunywa.

Staa wa muziki Frasha kutoka kundi la P-Unit Kenya

Frasha ambaye amekuwa akishirikisha mashabiki wake juu ya kila hatua ya mkakati huo, ametoa hamasa kwa watu kumuunga mkono, akieleza kuwa mabadiliko yanaanza kwa kuchukua hatua ndogo inavyowezekana.

Frasha kupitia kampeni hiyo mpya ya #100DAYSFREEOFALCOHOL, amewataka watu kutosita kumuunga mkono hata kama itakuwa wamepitwa kwa wiki nzima baada ya kampeni hiyo kuanza, zoezi ambalo pia linajenga na kuimarisha nidhamu binafsi.