Tuesday , 11th Aug , 2015

Staa wa muziki Feza Kessy, ameeleza kuwa mbali na muziki yeye anajishughulisha na ujasiriamali wa kuuza bidhaa mbalimbali, uigizaji, uandishi wa mashairi, pamoja na kazi kubwa ya malezi ya mwanae.

Staa wa muziki Feza Kessy

Staa huyo ambaye amezindua traki ambayo ni kolabo yake na Chegge ya 'Sanuka', siku ya jana, ameweka wazi kuwa, ikifika wakati sahihi ataweka wazi biashara zake kwa upande wa uigizaji, sasa hivi kazi kubwa iliyopo mbele yake ikiwa ni kusukuma muziki wake mbele.