Saturday , 23rd Apr , 2016

Msanii wa Bongo Flava Judith Wambura maarufu kama Lady JayDee ameweka hadharani maana ya ngoma yake mpya inayotesa mtaani kwa sasa kwa jina la NdiNdiNdi.

Akiitambulisha video ya wimbo huo kwa mara ya kwanza ndani ya FNL ya EATV Lady JayDee amesema kwamba maana ya wimbo huo ni 'The Ndi Mimi ni kitu Tori wewe si kitu' ili kuleta fleva ya muziki ndo akaiita NdiNdiNdi. 'Mimi ni kitu na wewe si chochote'.

Wimbo huo video yake imeruka kwa mara ya kwanza ndani ya FNL ambapo mashabiki wa Bongo Fleva walishiriki moja kwa moja kwa kumpongeza msanii huyo pamoja na kuuliza maswali mbalimbali ambayo aliyajibu papo kwa hapo.